Asante sana kwa kozi hii ya namna ya kujiajiri ,hakika nimepata maarifa muhimu ya namna ya kujiajiri kwenye kile ambacho nimeamua ambacho kujiajiri kwenye ardhi na majengo . Nakuhahidi sitakuangusha kwa kozi hii umewasha Moto wa kudumu kwenye safari ya kuelekea kwenye ndoto yangu . Kozi hii nimependa namna ulivyofundisha vizuri kwa njia ya audio na maneno yako yamebaki kichwani mwangu kama vile nilikuwa nasikiliza simulizi vile.Nitaendelea kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwako kama ninavyoendelea kujifunza kwenye vitabu vyako mbalimbali. Ningependa watu wangu wakaribu wajifunze kozi hii na vijana wote ,kwa maana vijana ni nguvu kazi ya taifa.Nitaendelea kusambaza vitabu vyako kwa watu wengi zaidi kwa kufanya hivyo nitakuwa nimesaidia wengi kupata maarifa yako. Kwa sasa Mimi ni wakala wa vitabu vyako Biharamulo kagera Patrick Edgar James Hitimisho:Nashukuru kwa ofa ya kozi hii kwa kuwa na gharama ndogo kuliko maarifa niliyopata.Hakika umejitoa kutusaidia wengi zaidi , mungu akuzidishie maisha marefu hili kusaidia wengi zaidi.