Karibu Retire Smart Skool, jukwaa ambalo limeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuwasaidia waajiriwa ā hususan watumishi wa umma na sekta binafsi ā kufanya uwekezaji wenye tija katika maeneo yenye hatari ndogo (vipande, hisa na hati fungani), na hivyo kuwawezesha kustaafu kwa furaha wakiwa na uhuru wa kifedha.
Kupitia jukwaa hili utaoneshwa kwa vitendo hatua kwa hatua jinsi ya:
- Kujenga tabia ya kuweka na kuwekeza akiba kwa kipato hichohicho ulichonacho sasa na kuchagua uwekezaji sahihi kulingana na umri na malengo yako
- Kufanya uwekezaji wenye usalama na faida endelevu
Manufaa ya kujiunga na jukwaa:
- Kutumia templates na zana rahisi kutumia kwa mahesabu na uchambuzi
- Kupata mifano halisi ya Tanzania ili kila hatua iwe ya vitendo
- Kushiriki kwenye Madarasa Maalum ya Uwekezaji na vipindi vya Live Q&A kwa msaada wa moja kwa moja
š” Tunageuza ndoto zako za ustawi wa kifedha kuwa mpango wa vitendo unaoweza kuanza leo.